RAGE AMGOMEA MALINZI, ASEMA HAKUNA MKUTANO SIMBA
Mwenyekiti wa Simba, Ismail Aden Rage akisoma mojawapo ya vipengele vya sheria katika katiba ya TFF.
Video wakati Aden Rage akiongea na wanahabari leo.
MWENYEKITI wa Simba Ismail Aden Rage amesikia taarifa aliyotumiwa na
Shirikisho la Tanzania (TFF) la kumtaka kuitisha mkutano mkuu wa dharura
wa klabu hiyo.Rage ametangaza msimamo wake huo leo ambapo amesema kamwe hawezi kuafiki kuchukua uamuzi huo kutokana na TFF kuingilia majukumu yake.
Rage amesema katiba ya Simba ibara ya 22 inaeleza wazi kwamba mwenyekiti akishirikiana na kamati yake ya utendaji wanaweza kuitisha mkutano mkuu wa dharura kama wataona kuna haja ya kufanya hivyo.
Amesema hakufurahishwa na uamuzi huo wa TFF ambapo alitegemea kwanza shirikisho hilo kupitia kamati yake ya utendaji inayoongozwa na Rais Jamal Malinzi lingekemea mapinduzi aliyofanyiwa.
“Katiba inatamka wazi mwenye mamlaka ya kuitisha mkutano mkuu ninayo mimi nikishirikiana na kamati ya utendaji na kwa jinsi hali ilivyo sioni haja ya kufanya hivyo, nasema hakuna mkutano,” alisema Rage.
Aidha Rage amesema endapo TFF itaendelea kumlazimisha kufanya hivyo hatasita kuchukua uamuzi mgumu wa kujiuzulu nafasi yake hiyo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni