Psy's Gangnam Style sio video inayotazamwa zaidi katika mtandao wa Yutube.
Wimbo huo maarufu kutoka Korea Kusini ulikuwa wimbo uliochezwa sana katika mtandao huo katika kipindi cha miaka mitano iliopita.Kanda hiyo ya video iliopata umaarufu hadi kuweka rekodi ya wimbo uliochezwa sana katika YouTube, hatua iliofanya kampuni hiyo kuandika alama mpya ya siri ya wimbo huo.
Lakini wimbo huo sasa umepitwa na kanda nyengine ya muziki wa Wiz Khalifa na Charlie Puth see you again.
Wimbo huo sasa umetazamwa mara 2,895,373,709 hivyobasi kuipiku idadi ya watazamaji 2,894,426,475 wa Psys.
Hiyo inaamanisha kwamba ''See You Again'' imetazamwa kwa jumla ya miaka 21,759.
Iwapo mtu mmoja angesikiza kila wimbo uliotazamwa katika mtandao huo wangeanza kusikiza wakati wa miaka ya barafu.
Wimbo huo uliandikiwa filamu Furious 7 ili kumuomboleza muigizaji Paul Walker aliyefariki katika ajali ya barabarani kabla ya filamu hiyo kukamilishwa.
Ikiwa na maneno ya kumuenzi Paul Walker{("it's been a long day without you my friend/ And I'll tell you all about it when I see you again"), Wimbo huo umekuwa ukipigwa sana katika mazishi nchini Uingereza.
Ulikuwa wimbo uliouza sana duniani 2015 na kupokea tuzo ya wimbo bora katika tuzo za Grammy na Oscars.
Kanda hiyo ya muziki inashirikisha eneo la mwisho la filamu ya Furious 7 ambapo waigizaji nyota Dominic Toretto {Van Diesel na O'Brien O'Conner{ Cody Walker anayechukua mahali pa nduguye Paul} wanaendesha gari sako kwa bako , wakitabasamu kwa mara ya mwisho kabla ya kuelekea katika barabara tofauti.
Huku kamera zikielekezwa juu mbinguni, kuna mshororo unaosoma: ''Ni ya Paul'' na kanda hiyo inaisha.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni