![]() |
Haruna Niyonzima |
Wachezaji watano
wameteuliwa kuwania tuzo ya Mchezaji Bora wa Ligi Kuu ya Tanzania kwa
msimu wa 2016/2017.Walioteuliwa kuingia kwenye kinyang'anyiro hicho ni
Aishi Manula (Azam FC), Haruna Niyonzima (Yanga), Mohamed Hussein
(Simba), Shiza Kichuya (Simba) na Simon Msuva (Yanga).
Simon Msuva kiungo mshambuliaji wa timu ya Yanga |
Wahusika watatumiwa fomu maalum za kupiga kura kwenye email za klabu zao na vyombo husika vya habari. Mwisho wa kupiga kura ni saa 6 usiku ya Jumanne, Mei 23 mwaka huu.
Hafla ya kutoa tuzo hiyo ambayo inaratibiwa na Kamati ya Ushauri ya Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) itafanyika Mei 24 mwaka huu kwenye ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.
Abou Coulibaly atachezesha mchezo wa pili wa Kombe la Mataifa ya Afrika kati ya Serengeti Boys ya Tanzania na Angola utakaofanyika Uwanja wa l'Amitie kuanzia saa 11.30 jioni kwa saa za Tanzania.
Mwamuzi Coulibaly atasaidiwa na Mamady Tere wa Guinea na Attia Amsaad wa Libya wakati mwamuzi wa akiba atakuwa Mohamed Maarouf wa Misri huku Kamishna akiwa ni Ismael Locate wa Reunion.
Aishi Manula |
"Angola ni wa kuchungwa sana. Kwa sababu walipocheza na Niger waliweza kusawazisha mabao mawili kipindi cha pili. Hii inaonesha kuwa ni wepesi wa kusoma makosa yao na kujirekebisha.
"Ila kikosi changu kiko imara, nikiamini kwamba kesho nitapata matokeo mazuri. Watanzania waendelee kutuombea. Tutafanikiwa," amesema Shime maarufu kwa jina la Mchawi Mweusi.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni