Msanii wa Marekani
Usher Raymond yuko ziarani nchini Tanzania akitembelea eneo la uhifadhi
wa wanyama pori la Serengti National Park.
Bwana Raymond alichapisha baadhi ya picha akiwa na familia yake katika akaunti yake ya Twitter.Alielezea hali ilivyo katika eneo hilo kama ya kufurahisha .
Ripoti za Usher Raymond kuzuru Tanzania zilisambaa kwa haraka nchini humo.
Vivutio vya kitalii nchini Tanzania kama vile mbunga ya uhifadhi wa wanyama pori ya Serengeti na mlima Kilimanjaro ni vivutio vinavyoongoza kwa utalii ambapo watu wengi maarufu wametembela.
SOURCE: BBCSwahili
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni