Chatu amshinda Mamba nguvu Australia
Chatu ameshinda vita vikali dhidi ya Mamba Kaskazini mwa mji wa QueensLand, kupigana na Mamba, kumpinda na kisha kumla.
Tukio hilo lilishuhudiwa katika ziwa Moondarra,
karibu na mlima Isa na kunaswa kwa kamera na wakazi wa eneo hilo siku ya
Jumapili.Nyoka huyo mwenye urefu wa futi 10, alijipinda kwa Mamba na kuanza kupambana naye majini.
Hatimaye, Nyoka huyo alifanikiwa kumshinda Mamba na kumtoa nje ya maji na kisha kumla.
"lilikuwa jambo la ajabu sana, '' aliambia BBC
"Tulimuona Nyoka akipambana na Mamba , alifanikiwa kumbana mamba hasa katika sehemu ya miguu ili kumdhibiti.''
"Pambano lilianzia ndani ya maji. Mamba alikuwa anajaribu kuweka kichwa chake juu ya maji wakati mmoja ingawa Nyoka alikuwa amembana sana.''
"Baada ya Mamba kufa Nyoka alijikunjua, na kuja mbele ya Mamba huyo na kuanza kumla,'' alisema Tifanny.
Bwana Corlis alisema kuwa ilimchukua nyoka muda wa robo saa kumla mamba huyo.
''Bila shaka Nyoka huyo alishiba vyema, na hatujui alikokwenda, baada ya mlo wake,'' alisema mama huyo ambaye hakutaka kusuburi kumuona Nyoka tena.
Mtu mwingine aliyeshuhudia pambano hilo Alyce Rosenthal, alisema kuwa wanyama hao wawili walipambana kwa karibu saa 5. Hatimaye wote walionekana wachovu.
''Sio kitu unachoweza kuona kila siku,'' alisema Alyce.
Source: BBC /Swahili
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni