YoungConcious™

Be Updated on the World of Sports, latest News and Entertainment Stories.

Propellerads

Translate

Welcome to Young concious .blogspot.com ==>>Feel free to leave your comment

Jumamosi, 11 Mei 2013

MTABIRI: MABOMU MENGINE YAJA

MNAJIMU maarufu nchini, Maalim Hassan
Yahya Hussein , amesema kuwa milipuko
zaidi ya mabomu itatokea nchini mwaka
huu.
Maalim Hassan ambaye ni mrithi wa kazi za
aliyekuwa mnajimu maarufu Afrika ,
marehemu Sheikh Yahya Hussein,
amefafanua kwamba milipuko mfano wa
ule uliotokea Arusha wikiendi iliyopita ,
itaitikisa nchi mwaka huu.
Alisema, jambo hilo alilitabiri mapema na
matokeo ndiyo yanaanza kuonekana,
akaongeza kuwa milipuko ya mabomu
inayokuja, italipua mpaka misikiti.
Maalim Hassan alisema, hali ya milipuko
itaendana na majanga , siyo Tanzania tu
bali duniani kote kwa sababu mwaka 2013 ,
ulianza katika siku mbaya kinyota.
“Mwaka 2013 ulianza Jumanne . Kinyota,
Jumanne ni siku ya mashaka , matatizo ,
vita, moto na malaika anayetawala siku
hiyo ni Israeli mtoa roho . Isitoshe mwaka
2013 namba 1 ni nyota ya punda ambayo
inawalenga viongozi , yaani watatofautiana
sana.
“3 ni nyota ya mapacha ambayo inaashiria
familia nyingi zitakuwa na matatizo , pia 1
ikijumlishwa na 3 inakuwa 4 ambayo ni
nyota inayowalenga wazazi yaani vifo vya
wajawazito vitakuwa vingi, ” alisema Maalim
Hassan na kuongeza:
“Yaani yanayotokea sasa ni sehemu ya
utabiri nilioutoa lakini bado mengine
yanaendelea, milipuko itaendelea kuwepo,
watu kuuana kwa risasi kwa sababu
Jumanne inatawaliwa na moto, hivyo watu
wanatakiwa kumuomba Mungu sana kwani
mwaka huu umeanza vibaya na siyo kwa
Tanzania tu mambo haya yatatokea duniani
kote.”
Kwa upande mwingine, Maalim Hassan
aliwaasa viongozi hususan wale wa kidini,
kuwa makini na kauli zao , vinginevyo
zinaweza kuleta mifarakano ya kijamii
kupitia imani zao .
“Kwa Waislamu na Wakristo, hekima na
busara zitumike katika kuzungumzia
mambo yanayoendelea , kwani kauli za vita
zimekuwa zikitajwa sana na baadhi ya watu
katika jamii tofauti na miaka iliyopita,
hivyo umakini unatakiwa kuwa wa hali ya
juu kwa viongozi ili kuepusha vita
Tanzania ,” alisema.
Kauli hiyo ya Maalim Hassan kuhusu
marejeo ya utabiri wake alioutoa mapema
mwaka huu, imekuja muda mfupi baada ya
mlipuko wa bomu kwenye Kanisa la
Mtakatifu Joseph Mfanyakazi, Parokia ya
Olasiti, Arusha , lililoua watu watatu na
kujeruhi wengine zaidi ya 70, pamoja na
kusababisha uharibifu mkubwa wa mali,
Jumapili iliyopita.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

Propellerads