YoungConcious™

Be Updated on the World of Sports, latest News and Entertainment Stories.

Propellerads

Translate

Welcome to Young concious .blogspot.com ==>>Feel free to leave your comment

Jumamosi, 11 Mei 2013

DAAH!

DAAH! Pati ya kuzaliwa ‘bethidei ’ ya mtoto
wa Irene Pancras Uwoya na mumewe
Hamad Ndikumana ‘Kataut ’, Krrish
imekuwa kama ya harusi , kwa namna
ilivyofanyika, Risasi Jumamosi lina kila kitu.
JB akifungua Shampeni
Staa huyo wa filamu za Kibongo aliangusha
bonge la sherehe kwenye Ukumbi wa
Shekinah, Makonde , Mbezi Beach jijini Dar,
Jumatano iliyopita na kuhudhuriwa na
mastaa lukuki .
Uwoya Ndiku na Krrish Full Furaha
Krrish alikuwa akitimiza miaka miwili tangu
alipozaliwa Mei 8 , 2011 ambapo sherehe
ilianza mchana hadi usiku mnene kukiwa
na kila aina ya burudani hivyo kuwaacha
watu midomo wazi kufuatia kufuru hiyo.
Uwoya,Ndiku wakikata Keki kwa pamoja
na mtoto wao Krrish
MAAKULI MWANZO MWISHO
Kwa mujibu wa ‘balozi’ wetu , wageni
waalikwa walipoanza kuingia ndani ya
ukumbi, walikuwa wakikaribishwa kwa
vinywaji vya kila aina na chakula
kilichotengenezwa kwa utaalam wa hali ya
juu hata kabla pati hiyo haijaanza rasmi,
zoezi ambalo liliendelea hadi mwisho .
Muonekano wa keki
WATOTO WATENGENEZEWA KAMA
HOLLYWOOD
Katika shughuli hiyo , kulikuwa na michezo
mbalimbali ya kisasa ya watoto walioalikwa
ambao walijengewa vijumba ‘spesho ’ vya
kuchezea kama Hollywood, Marekani.
Shamsa Ford na Welu Sengo wakijiachia
ULINZI MKALI
Ili kuhakikisha kuwa hakuna kitu
kinachoweza kuleta ‘mizinguo ’ na
kuhatarisha burudani, kulikuwa na
mabaunsa wapatao saba waliokuwa
wameweka ulinzi mkali.
UWOYA , NDIKU
Huku watu wakiendelea kugonga ‘mpunga ’,
vinywaji na muziki, waliingia wazazi wa
Krrish, Uwoya akifuatana na Ndiku wakiwa
wamembeba mtoto wao na kusababisha
shangwe za makofi na vigelegele.
MAPENZI MOTOMOTO
Uwoya na Ndiku , muda wote walionekana
wakiwa katika mapenzi motomoto kwa
kukimbizana ukumbini kwa mabusu ya
kumwaga .
BONGO MOVIES
Katika mnuso huo, mastaa mbalimbali
kutoka Bongo Movies walipoingia ukumbini
walichangamsha sherehe kwani mara zote
walikuwa wakifurahi na kuserebuka muziki .
JB AFUNGUA SHAMPENI
Kulikuwa na shampeni zipatazo arobaini
ndani ya ukumbi huo lakini Steven Jacob
‘ JB’ aliombwa kufungua moja kwa ajili ya
kuziwakilisha nyingine huku watu
wakimuimba; ‘ Bonge la Bwana ’ na
kumfanya kuona soo kimtindo .
BIBI , BABU KRRISH
Chereko zilikolea baada ya baba na mama
mzazi wa Uwoya , kujichanganya na wageni
waalikwa huku wakicheza na kufurahi kwa
pamoja.
WATOTO YATIMA
Ili kuonesha anajali watoto wengine ambao
wazazi wao wametangulia mbele ya haki,
staa huyo aliwaalika watoto yatima ili
kusherekea na Krrish siku hiyo .
Hadi Risasi Jumamosi linaanua jamvi
ukumbini hapo usiku, watu walikuwa
wakiendelea kutandika ‘masanga ’ na
kuserebuka muziki .

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

Propellerads