Na Erick Evarist
HABARI zilizonaswa na Amani zinaeleza
kuwa nyota wa sinema Bongo , Elizabeth
Michael ‘ Lulu’ , ameitwa katika Jiji la Dubai,
Falme za Kiarabu kwa ajili ya kula ‘ bata’
ikiwa ni pole yake kwa kusota Gereza la
Segerea kwa karibu mwaka mmoja .
Elizabeth Michael ‘Lulu ’
Chanzo makini kilipenyeza habari kuwa
mapedeshee hao wamemualika staa huyo
huku ikinyetishwa kwamba , vigogo wa
sanaa hiyo Bongo , Steven Mengere ‘Steve
Nyerere’ na Mahsein Awadh ‘Dk . Cheni’
ndiyo watakaomsindikiza .
“Mapedeshee wamemtumia mamilioni ya
fedha Lulu , wanataka kufanya naye pati ya
pamoja kwa vile ni miongoni mwa mastaa
wa Bongo wanaokubalika nchini humo na
pia kumpa pole kwa kukaa gerezani muda
mrefu.
“Mbali na sherehe hiyo , watakapokuwa
nchini humo wanatarajia kuendeleza filamu
ambayo wameanza kuirekodi hapa Bongo, ”
kilisema chanzo hicho.
Hata hivyo, chanzo kiliweka wazi kwamba
kwa sasa , Lulu si rahisi kusafiri nje ya
Bongo kwa vile kesi aliyonayo ina mipaka
ya sehemu za kwenda.
Alipotafutwa Dk . Cheni juu ya ishu hiyo,
alisema waliomuita Lulu si mapedeshee
bali ni Wabongo waishio kule, lakini
masharti ya kesi yake hawezi kusafiri nje
ya Tanzania .
Dk. Cheni akaulizwa kuhusu yeye na Steve
Nyerere kuwepo kwenye safari hiyo
ambapo alisema hana ufafanuzi zaidi ,
akakata simu .
Amani lilimsaka Steve Nyerere ili naye
aweze kutoa ufafanuzi juu ya madai hayo
lakini Jumanne , simu yake ya mkononi
ilikuwa haipatikani.
Kwa upande wake , Lulu hakuweza kusema
lolote, sharti ambalo amewekewa na watu
wake wa karibu baada ya kuachiwa kwa
dhamana kufuatia kesi yake ya kumuua bila
kukusudia aliyekuwa nyota wa filamu za
Bongo, marehemu Steven Kanumba.
Translate
Jumamosi, 11 Mei 2013
About Young Concious
Soratemplates is a blogger resources site is a provider of high quality blogger template with premium looking layout and robust design. The main mission of templatesyard is to provide the best quality blogger templates.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni