Klabu ya Manchester City imepanda hadi nafasi ya tatu katika jedwali la ligi ya Uingereza baada ya kuishinda Leicester City.
Hathivyo
City walinusurika baada ya refa Bobby Madley kukataa bao la penalti
lililofungwa na Riyad Mahrez ambaye alikuwa ameangushwa na Gael Clichy.Mahrez alikuwa na fursa ya kufanya mabo kuwa 2-2 lakini akateleza alipopiga mkwaju huo na kuugusa mpira na mguu wake wa kulia baada ya kuupiga na mguu wake wa kushoto.
Mpira ulikuwa tayari umeingia wavuni pale refa alipokataa ba hilo na kuipatia Manchester City mpira wa adhabu kuekekezwa lango la Leicester hatua iliowapatia afueni Mkufunzi Guardiola na wachezaji wake..
Citu walitawala kipindi kirefu cha mchezo katikia uwanja wa Etihad na walikuwa wanakaribia ushindi walpokuwa kifua mbele kqwa 2-0.
Lakini mlinzi wa Leicester Okazaki aliipatia klabu yake bao zuri baada ya kuvamia ngome ya Manchester City.
Mabao ya City yalifungwa na de Jesus kwa mkwaju wa penalti na Silva .
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni