![]() |
| Wachezaji wa klabu ya simba |
Klabu maarufu ya
kandanda nchini Tanzania, Simba, imepata udhamini wa miaka mitano kutoka
kwa kampuni ya SportPesa ambayo wiki hii imezindua rasmi uchezaji wa
kamari kwa kubashiri matokeo ya kandanda nchini humo.
Udhamini huo
wa donge nono ulitangazwa wakati wa mechi ya ligi ya Vodacom kati ya
Simba aka Wekendu wa Msimbazi na Stand United ya Shinyanga katika
uwanja wa kitaifa jijini Dar es Salaam.Akizungumza katika uwanja huo, mkurugenzi wa usimamizi wa SportPesa nchini Tanzania Abbas Tarimba amesema huo ndio mwanzo tu, na kwamba timu zingine zitafaidika kwani kampuni hiyo inataka kubadilisha kabisa sura ya michezo nchini Tanzania.
``Tutafanya mpango wa mechi za kirafiki kati ya Simba na timu kubwa za nga'mbo tukitumia ushirikiano wetu na vilabu vya England kama vile Hull City, Arsenal na Southampton lengo kubwa likiwa ni kuwapa wachezaji wa Simba nafasi ya kucheza kandanda Ulaya,'' amesema Tarimba.
![]() |
| Klabu maarufu ya kandanda nchini Tanzania, Simba, imepata udhamini wa miaka mitano kutoka kwa kampuni ya SportPesa |
Miongoni mwa walioshudia hafla hiyo ni mkurugenzi mkuu wa SportPesa nchini Tanzania, Pavel Slavkov, Tarimba na Rais wa Simba Evans Elieza Aveva na mdogo wake Geoffrey Nyange Kaburu.



Hakuna maoni:
Chapisha Maoni