Mwanamke mmoja wa
umri wa miaka 23 nchini India amekata uume ya wa kiongozi mmoja wa dini
kwenye jimbo lililo kusini mwa nchi la Kerala, akidai kuwa alimbaka kwa
miaka kadha.
Polisi wanasema kuwa kiongozi huyo wa dini kwa jina
Gangeshananda Theerthapada, alikuwa akienda kwenye nyumba ya mwanamke
huyo kufanya maombi kwa ajili ya afya ya babake.Hii ni baada ya mamayake kuwa na matumaini kuwa mtu huyo ya Mungu angetatua matatiza ya familia yake.
Badala yake binti yake alidai kuwa alimdhulumu kingono kila mara.
Siku ya Ijumaa usiku alichukua kisu na kumshambulia wakati alijaribu kumbaka na kisha kuwaita polisi mwenyewe.
![]() |
Mwanamke akata uume wa kiongozi wa dini India |
Hospitali hiyo ilisema mwanamume huyo wa miaka 54 kutoka Kollam alilazwa kwenye hospitali hiyo .
Uume wake ulikuwa umekatwa kwa asilimia 90 na hakuna uwezekano kuwa ungerudishwa tena..
Madaktari walijaribu kuzuia kufuja kwa damu na kumfanyia upasuaji ili aweze kupitisha mkojo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni