![]() |
Marufuku ya uuzaji wa nyama ya mbwa yazuia wasiwasi katika hafla ya Yulin China |
Sherehe ya kula
nyama ya mbwa nchini China ilio na umaarufu kwa ukatili wa wanyama mwaka
huu itapigwa marufuku kuuza nyama ya mbwa.
Ulaji wa mbwa nchini
China sio haramu na wauzaji wa nyama hiyo tayari wameanza kulalamikia
marufuku hiyo wengine wakisema hawajaisikia .Sherehe hiyo inayofanyika mwezi Juni kila mwaka imekuwa ikivutia pingamizi kubwa kutoka kwa wanaharaki wa wanyama wanaosema kuwa wanyama hao hufanyiwa ukatili.
Inakadiriwa kuwa katika sherehe hiyo ya Yulin iliofanyika miaka michache iliopita, takriban mbwa na paka 10,000 walichinjwa na kufanywa kitoweo wakati wa sherehe hiyo ya siku kumi.
Lakini idadi hiyo imekuwa ikipungua katika siku za hivi karibuni huku pingamizi ikiendelea nchini China na kimataifa.
Wanaharakati kadhaa wa wanyama wanasema kuwa wauzaji na mikahawa wameambiwa kwamba hakuna nyama ya mbwa itakayouzwa wakati na kabla ya sherehe hiyo.
Peter Li, mtaalamu wa sera za China aliambia BBC kwamba mamlaka tayari imejaribu kuwakatisha tamaa wanaotekeleza hatua hiyo ,na kwamba mwaka huu itawapiga faini watakaokiuka marufuku hiyo.
![]() |
Raia wa China wakila nyama ya mbwa wakati wa sherehe ya Ylin nchini humo |
Lakini marufuku hiyo itakuwa ya muda ikimaanisha kwamba mbwa wengi wanaweza kuchinjwa kabala ya sherehe hiyo.
''Bado kuna pingamizi kutoka kwa wafanyibiashara wa nyama hiyo ya mbwa'', alisema bwana Li.
''Kote nchini walikuza ulaji wa nyama ya mbwa kama utamaduni wa kitaifa pamoja na chakula cha Wachina.
Hilo sio la kweli ,baraza la mji wa Yulin haliweza kufanya kitu kama hicho kwa kuwa kitasababisha wasiwasi mkubwa kwa kijamii.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni