![]() |
Tuhuma ya Urusi kuingilia uchaguzi wa Marekani imegonga vichwa vya habari duniani kwa muda sasa |
Rais wa Marekani
Donald Trump amesema anataka kuanza kuendesha nchi baada ya utawala wake
kugubikwa na utata wa tuhuma za timu yake ya kampeni kushirikiana na
Urusi.
Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari
Washington, akiwa pamoja na Rais wa Colombia ambae yuko ziarani nchini
Marekani, amesema anaheshimu uteuzi wa mchunguzi maalumu, lakini
akarudia kusema kuwa sakata hilo linaigawa nchi:Rais Trump pia amekana kujaribu kuishawishi FBI katika uchunguzi wake kwa kumfuta kazi mkurugenzi wake James Comey.
Amemwelezea Comey kuwa hakuwa chaguo la watu.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni