Mgombea wa urais
nchini Marekani kwa tiketi ya chama cha Republican Donald Trump ameahidi
kubadilisha sifa zake katika mkutano wa faragha na viongozi wa
Republican.
Mfanyibishara huyo ambaye yuko kifua mbele katika
kuwania urais kupitia chama hicho alitoa ujumbe wake kupitia wasaidizi
wake ,kulingana na chombo cha habari cha AP.Kuimarika kwake katika mchujo huo kufikia sasa kumetuma ishara miongoni mwa viongozi wa chama hicho kwamba matamshi pamoja na sera zake huenda zisiwavutie wapiga kura.
Majimbo matano yanapiga kura siku ya Jumanne kumchagua mgombea wao wa urais.
Bwana Trump ana uongozi mkubwa wa idadi ya wajumbe lakini huenda asipate wajumbe 1,237 anaohitaji kushinda mchujo huo bila ya mkutano wa wanachama.
Wasaidizi wamewaambia viongozi wa chama kwamba amekuwa akibadilisha sifa zake na kwamba hatua hiyo imeanza kufua dafu.
Source:BBCSwahili
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni