| dola vimepitisha ukuzaji wa vyakula katika eneo hilo la Fukushima ,wenyeji wengi wamesusia kula vyakula vilivyokuzwa huko wakihofia kuathirika na miale ya nyuklia |
Katika Jaribio la kwanza katika wilaya ya Ojima mimea 2,000 aina ya 'ornamental anthurium' ilimea kwa njia nzuri na kuwaridhisha watafiti, jarida la Asahi Shimbun limeripoti.
Wilaya hiyo ya Ojima iliyoko takriban kilomita 50 kutoka kiwanda kilichoathirika vibaya zaidi cha nyuklia cha Fukushima Daiichi.
Kiwanda hicho kiliyeyuka baada ya tetemeko kubwa la ardhi kukumba eneo hilo na kusababisha mafuriko.
| Kiwanda hicho kiliyeyuka baada ya tetemeko kubwa la ardhi kukumba eneo hilo na kusababisha mafuriko. |
Wengi wao hawaamini vipimo vilivyotolewa na wizara ya afya kuwa ni salama kula vyakula hivyo kuwaacha wakulima wengi wakiwa hawana wateja wa vyakula vyao.
''kwa kutumia mchanga huu wa bandia,tunatarajia wakulima wa Fukushima huenda wakafufua biashara yao ambayo imeathirika sana na uvumi wa kuwepo kwa miale ya nyuklia yenye sumu.'' alisema Profesa Takahiro Hayashi kutoka chuo kikuu cha Kinki.
Chuo hicho ndicho kinachoendesha utafiti huo wa mchanga bandia.
| Wakulima katika mji wa Fukushima Japan eneo lililoathirika na kuyeyuka kwa tanuri ya nyuklia mwaka wa 2011 wamegundua njia mbadala ya kukuza mazao |
''Nia yangu ni kushuhudia maua kutoka Fukushima ikituzwa washindi wa michezo mbalimbali katika mashindano ya Olimpiki ya 2020 inayoratibiwa kufanyika mjini Tokyo Japan.'' aliongezea Takahashi.
Source:BBCSwahili

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni