- 22 Aprili 2016
Mwanamume
aliyefariki ameteuliwa kusimamia mechi ya soka nchini Nigeria ambayo
itachezwa Jumapili, mwandishi wa BBC anayefuatilia masuala ya soka
Oluwashina Okeleji anasema.
Wale Akinsanya aliteuliwa kuwa mwamuzi
kwenye mechi baina ya Warri Wolves na Giwa FC katika mji wa Warri
kusini mwa Nigeria, gazeti la Punch la Nigeria limeripoti.Hii ni licha ya kwamba Akinsanya alifariki tarehe 22 Januari 2016 wakati wa kufanywa kwa mtihani wa Fifa Cooper Test, ambao hutumiwa kuamua iwapo marefarii wanatosha kuendelea kusimamia mechi.
Aliteuliwa kusimamia mechi hiyo na mrengo wa Shirikisho la Soka la Nigeria (NFF) unaoongozwa na
Chris Giwa
Source: BBCSwahili
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni