Homa na mitetemo ya hasira kwa Wananchi wanaofatilia siasa hasa kwenye chaguzi kuu za nchi huwa ipo kila tukio hili kubwa linapofanyika, kuona watu wamepigana, kutoa lugha nzito au kuonyesha hisia zao za kumpinga mgombea flani moja kwa moja ni vitu vinavyotokea kwenye chaguzi kuu.
Mgombea Urais kwenye uchaguzi mkuu wa Marekani Donald Trump alikoswakoswa kushambuliwa na mmoja wa Wananchi waliokusanyika kumsikiliza kwenye mkutano wake wa kampeni huko Ohio ambapo wakati jamaa huyo aliporuka uzio ili kwenda kumfataTrump jukwaani, walinzi walimdaka mapema hivyo hakufika kwenye jukwaa.
Polisi walimkamata huyo jamaa aitwae Thomas Dimassimo (22) lakini aliachiwa saa kadhaa baadae, unaweza kutazama hii video hapa chini kuona ilivyokuwa…
VIDEO NYINGINE NI HII HAPA CHINI…
Thomas Dimassimo aliendelea kuandika matusi kwa Trump baada ya kuchiwa kwa dhamani siku ya tukio na kukanusha pia kwamba alikua anakwenda kumshambulia kwa kisu jukwaani, alisema hakuwa na silaha yoyote ya kumdhuru Trump.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni