Daktari moja wa meno mholanzi ameshtakiwa kwa kuwakata midomo zaidi ya wateja wake 100 maksudi.
"Dentist of Horror" anakabiliwa na mashtaka nchini Ufaransa.Daktari huyo anayefahamika kwa majina kamili ya Jacobus van Nierop, anakabiliwa na mashtaka ya kung'oa meno yenye afya kwa kisingizio tu.
Nierop anasemekana kuwajeruhi vibaya wagonjwa wake katika kliniki yake iliyoko katika kijiji kimoja cha Ufaransa.
Baadhi ya wagonjwa wake walishikwa na maradhi ya ufizi yaliyosababisha midomo yao kuoza huku wengine wakiambukizwa maradhi yaliyotumbua usaa midomoni mwao.
Mahakama iliambiwa kuwa mwanamke mmoja aliyekwenda katika zahanti hiyo akitaka meno yake yanyooshwe, nusura abakie kibogoyo.
Daktari huyo alitorokea Canada alipogundua anatafutwa na maafisa wa polisi.
Sasa amerejeshwa Ufaransa alikotekeleza unyama huo ili haki itendeke.
Endapo atapatikana na hatia, Daktari Jacobus van Nierop, huenda akafungwa jela kwa miaka 10.
Source: BBCSwahili
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni