YoungConciousâ„¢

Be Updated on the World of Sports, latest News and Entertainment Stories.

Propellerads

Breaking News

Translate

Welcome to Young concious .blogspot.com ==>>Feel free to leave your comment

Jumanne, 8 Machi 2016

Ajificha(Azamia) ndani ya ndege ya Ethiopia hadi Sweden

Ajificha ndani ya ndege ya Ethiopia hadi Sweden



Maafisa nchini Sweden wanachunguza kisa cha mwanamume mmoja ambaye alipatikana amejificha katika sehemu ya mizigo ya ndege iliyotoka jijini Addis Ababa, Ethiopia kuelekea mji mkuu wa Stockholm.
Mwanamume huyo anaaminika alijificha katika ndege hiyo ya Ethiopian na kusafiri kwa takriban saa nane.
Aligunduliwa Jumatatu, ndege ilipotua katika uwanja wa Arlanda mjini Stockholm.
Maafisa wa polisi nchini Sweden wanasema mwanamume huyo ameomba hifadhi nchini humo na kwamba hali yake ya kiafya iko shwari kwa sasa.
Hata hivyo wameanzisha uchunguzi kubaini iwapo alishirikiana na mhudumu wa ndege hiyo kwa mujibu wa msemaji wa polisi nchini Sweden Kgell Lendgren.
''Tutatuma maswali yetu kwa utawala wa uwanja wa ndege na wamiliki wa ndege hiyo ya Ethiopia Airline:
''Tungetaka kujua aliwezaje kuingia ndani ya ndege hiyo, Makasha haya yaliwekwa wakati upi ndani ya ndege hiyo ?''
''Na ni nani aliyepakia mzigo wa ndege hii, ? '' Haya ndio baadhi ya maswali ambayo yanahitaji majibu ya haraka.
Shirika la ndege la Ethiopia limesalia kimya kuhusiana na tukio hilo nadra.
Katika mji mkuu wa Ethiopian, Addis Ababa, maswali mengi yanahitaji majibu.
Hii sio mara ya kwanza kwa tukio kama hilo kutokea, Mwaka wa 2014 mwanaume mwengine ambaye baadaye aligunduliwa kuwa mfanyikazi wa ndege hiyo alikwenda hadi katika uwanja wa ndege wa Stockholm na kuomba uhifadhi.

Source: BBCSwahili

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

Propellerads