Kampuni ya Hummel imetangaza
ushirikiano mpya na shirikisho la soka nchini Afghanistan katika mpango
ambao pia utasaidia kikosi cha taifa cha timu ya soka ya wanawake
waliovalia hijab ambazo hutengezwa na kuwa katika vazi la michezo.
Kampuni
hiyo ya jezi za michezo ya Denmark ilichaguwa siku ya kimataifa ya
wanawake kuzindua vazi hilo jipya la wanawake litakaloorodhesha hijab
ikiwa ni juhudi ya kuwavutia wanawake wengi ili kuweza kushindana na
wanawake wenzao kimataifa.Ubunifu huo unashirikisha turathi za Afghanistan na utamaduni huku hijab ikiwa kinguo kitakachowaruhusu wanawake kufunikwa kutoka kichwani hadi miguuni bila ya kuathiri uwezo wao wa kucheza.
Hatua hiyo ni ya kwanza kwa jezi ya michezo kushirikisha hijab.
Mmiliki wa Hummel Christian Stadil amesema kuwa chapa hiyo inaamini kwamba iwapo unataka kufanya mabadiliko muhimu,ni sharti ukutane na mataifa pamoja na utamaduni ulipo.
Source: BBCSwahili
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni