Kampuni ya Nike
imesimamisha kwa mda uhusiano wake na bingwa mara tano wa tenisi Maria
Sharapova baada ya mchezaji huyo kukiri kupatikana na dawa za kusisimua
misuli.
Kampuni hiyo imesema kuwa imeshangazwa na kukiri kwake kwamba
alipatikana na dawa hizo katika michuano ya Australia Open mnamo mwezi Januari.''Tumeamua kusitisha uhusiano wetu kwa mda huku uchunguzi ukiendelea ,ilisema.Tutandelea kuangalia hali ilivyo''.
Uhusiano wa Sharapova na Nike ulianza akiwa miaka 11.
Bi Sharapova ndiye mchezaji wa kike anayelipwa fedha nyingi baada ya kupokea dola milion 30 mwaka 2015 kutokana na ushindi pamoja na ufadhili kulingana na Forbes.
Hii inashirikisha kandarasi na Evian ,Tag Heur,Porshe.
Source:BBCSwahili

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni