Ligi kuu ya Tanzania bara iliendelea siku ya Jumatano kwa michezo minne kupigwa
katika dimba la Mkwakwani mkoani Tanga , Coastal Union waliibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Mgambo Jkt.Tanzania Prison wakicheza katika uwanja wao wa nyumbani wa Sokoine walitoshana nguvu na Kagera Sugar kwa kufungana bao 1-1.
Nao Mwadui Fc wakikipiga na Majimaji wametoshana nguvu kwa sululu ya 0-0,JKT Ruvu wakawachapa Toto African kwa mabao 2-0.
Ligi hiyo itaendelea tena hapo kesho kwa Simba kucheza na Ndanda FC,Mbeya City watawaalika Staind United, katika dimba la Sokoine.
Source: BBCSwahili
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni