YoungConciousâ„¢

Be Updated on the World of Sports, latest News and Entertainment Stories.

Propellerads

Breaking News

Translate

Welcome to Young concious .blogspot.com ==>>Feel free to leave your comment

Alhamisi, 10 Machi 2016

Umeisikia hii ya mtoto mdogo kusafirishwa ndani ya begi kama Mzigo!?.....Bofya hapa sasa kupata habari

Abiria ndani ya ndege ya Air France

Mwanamke mmoja alisafiri kwa ndege kutoka Istanbul nchini Uturuki hadi mjini Paris akiwa na mtoto aliyemficha ndani ya begi lake la mkononi,shirika la ndege la Air Ufaransa limesema.
Shirika hilo limesema kuwa mtoto huyo aliyesafiri bila kulipa nauli alipatikana ndani ya ndege hiyo siku ya Jumatatu usiku.
Duru katika shirika hilo iliambia shirika la habari la AFP kwamba mwanamke huyo ni mkaazi wa Ufaransa ambaye alikuwa katika harakati za kumfanya mtoto huyo kutoka Haiti kuwa wake.
Shirika hilo la ndege lilielezea mamlaka ya Ufaransa lakini waendesha mashtaka wakaamua kutofungua mashtaka.
Mwanamke huyo alikuwa akingoja kuchukua ndege nyingine mjini Istanbul lakini akazuiliwa kupanda ndege hiyo na mtoto huyo ,duru hiyo iliarifu AFP.


Ndege ya kampuni ya Air France

 
 
Alinunua tiketi nyingine na kumficha mtoto huyo ndani ya begi.
Alipokuwa ndani ya ndege hiyo ,alimweka mtoto huyo katika miguu na kujifunika na blanketi ,lakini mtoto huyo wa kike alitaka kwenda haja na alionekana na abiria wengine.
Haijulikani mtoto huyo alikuwa na miaka mingapi ,duru moja ilieleza kwamba alikuwa na miaka minne huku nyingine ikisema alikuwa na mwka mmoja ama miwili hivi.

Source: BBCSwahili

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

Propellerads