Mnigeria mmoja ameuliwa na
rafiki yake huko Mumbai juzi jumamosi usiku kufuatia kubishana nani
mchezaji bora kati ya Cristiano Ronaldo na Lionel Messi
Kwa maelezo ya Polisi,
Obina Michael Durumchukwa,34,alikuwa anasheherekea siku yake ya kuzaliwa
akiwa na rafiki yake Nwabu Chukwuma,22, na baadaye wakaingia katika
ubishi huo wa nyota hao wawili.
Polisi huyo, Kiran Kabadi
amesema kuwa,Durumchukwa alianza kurusha glasi kwa Chukwuma, akamkosa na
kugonga ukutani, Chukwuma akachukua vile vipande vya glasi na kurusha,
vikamchana Durumchukwa kwenye koromeo
Baada ya tukio hilo Chukwuma amekamatwa na Polisi kwa kosa la Mauaji. .
Source: Bloguyawananchi
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni