Mshambuliaji wa kimataifa wa Brazil anayeichezea klabu ya FC Barcelona ya Hispania Neymar, February 2 amerudi kwenye headlines juu ya zile stori za dau la usajili wake, Neymar kaitwa mahakamani kutoa ushahidi kuhusu usajili wake wa kutoka Santos kujiunga na FC Barcelona mwaka 2013.
Klabu ya Santos ya Brazil wanawatuhumu Neymar na baba yake kudanganya kuhusu dau la usajili. Muwakilishi wa Santos Fatima Cristina Bonassa anaeleza kuwa Neymar wakati anajiunga na FC Barcelona alikuwa mtu mzima na anafahamu kila kitu kilichokuwa kinaendelea.
Bonassa alisikilizwa kwa masaa matano na jaji José de la Mata na kuilaumu kampuni ya Kibrazil ya Brazilian investment fund DIS ambayo ilikuwa ina miliki asilimia 40 haki za Neymar wakati yupo Santos. Usajili wa Neymar kutoka Santos kwenda FC Barcelona unatajwa kuwa wa pound milioni 43, pound milioni 30 zimeenda katika kampuni ya N&N inayomilikiwa baba yake Neymar na pound milioni 13 kwenda Santos, lakini dau linatajwa kuwa pound milioni 63, tukio ambalo linafanya kuwepo na kesi mahakamani.
Source:MillardAyo
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni