Kutokana na kitu ‘selfie’ kuonekana kupata nguvu kubwa sana na kupendwa na watu wengi, yako matatizo pia ambayo yanasababishwa na selfie hizohizo, ishu ya ajali na vifo nayo inatajwa.
Wiki chache zilizopita nilikusogezea stori kutoka India kuhusu msichana mmoja kufariki baada ya kuanguka akiwa anajipiga ‘selfie’ kwenye ukingo wa bahari.
Ya leo inahusu kijana wa miaka 16 ambaye amegongwa na treni ya abiria na kufariki India wakati akijipiga selfie mbele ya treni, ishu yote ni kwamba alisimama kwenye reli akisubiri treni ifike karibu zaidi ili apige selfie.
Ripoti ya ajali zilizotokana na ‘selfie’ inaonesha mwaka 2015 watu 27 walifariki kwa kujitega ili wajipige selfie, nusu ya watu hao waliofariki ni watu wa India ikafikia wakati wakayataja maeneo 16 ambayo ni marufuku kupiga selfie.
Source: Millardayo
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni