YoungConciousâ„¢

Be Updated on the World of Sports, latest News and Entertainment Stories.

Propellerads

Breaking News

Translate

Welcome to Young concious .blogspot.com ==>>Feel free to leave your comment

Jumanne, 2 Februari 2016

John Terry kuthibitisha kuondoka Chelsea.....Habari kamili click hapa kupata zaidi



Beki wa kati na nahodha wa klabu ya Chelsea John Terry amethibitisha kuwa hatoendelea kuitumikia Chelsea na mwisho wa msimu huu ndio mwisho wake Chelsea na sasa hataki kuichezea club yoyote ya Uingereza bali anataka kwenda kucheza mbali kwengine.
John Terry mwenye umri wa miaka 35 ataondoka Chelsea July mwaka huu ikiwa ni miaka 21 imepita toka ajiunge na timu hiyo akiwa na umri wa miaka 14 ambapo Kurt Zouma ambaye amekuwa akicheza na John Terry msimu huu baada ya kufikiwa na hizi taarifa amehuzunishwa kuondoka kwa Terry na kukumbushia kuwa hata Drogba aliumia pia.
Ramacv
Kiukweli nimeshangazwa na sikulitegemea hili kutokea, kwa sasa tunalazimika tu kuangalia ni kipi John Terry atafanya, kwa sababu mimi nilitegemea kuwa atacheza Chelsea kwa mwaka mmoja au miwili zaidi, hii inafanya nijihisi kuwa tumempoteza Drogba, msimu uliopita, kiukweli Terry ni mtu muhimu Chelsea na sijui nafasi yake inazibwa vipi” >>> Kurt Zouma
Terry ambaye alikuwa na matumaini ya kupewa mkataba wa mwaka mmoja mbele, atakuwa anaungana na mastaa wenzake wa zamani wa Chelsea Didier Drogba na Frank Lampard ambao waliondoka pia Chelsea ambapo Terry amedumu Chelsea kwa miaka 21 na amefanikiwa kucheza jumla ya mechi 696 akiwa na klabu hiyo.
Toka mwaka 2014 Terry ameongeza mkataba wa mwaka mmojammoja Chelsea ikiwa ni utaratibu wa club hiyo kutoa mkataba usiozidi mwaka mmoja kwa Wachezaji wenye umri zaidi ya miaka 30.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

Propellerads