Kila jamii ina tamaduni zao katika ulaji
wa vyakula na kuna nchi za wenzetu ulaji wa nyama ya mbwa, panya si
kitu kigeni kwao na hutumia kama kitoweo kila siku lakini kwa wengine
huona ni jambo la ajabu na haramu kwao kutumia.
Kuna stori kutoka Nigeria kwenye mji wa Anambra ambapo Mgawaha mmoja umedaiwa kuwauzia wateja wao nyama za binadamu tena kwa bei kubwa tofauti na bei nyingine.
Inasemekana
Polisi walipewa taarifa hizo na kuamua kufanya uchunguzi na ndipo
walipovamia mgahawa huo na kukuta vichwa viwili vya binadamu vikiwa
ndani ya mfuko na tayari vimekatwa.
Mmoja
wa watu waliopokea kwa mshtuko mkubwa taarifa hizo ni mchungaji mmoja
ambaye aligundua amekula nyama isiyo ya kawaida na kuwa wa kwanza
kuwataarifu Polisi ambao walifika na kubaini kuwepo kwa uuzaji huo.
Kwa sasa mgahawa huo umefungwa na wahusika 11 wanashikiliwa na Polisi kwa ajili ya uchunguzi zaidi.
Source: MillardAyo
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni