Kesi
za watu kujipiga risasi sio ngeni kusikika na mara kwa mara, zimekuwa
zikitokea sehemu mbalimbali duniani kutokana sababu mbalimbali ambazo
hufikiwa na walengwa.
Hii imetokea kule Hispania baada ya
jamaa kukaa na kafikiria ni kwa nini asijaribu kujipiga risasi ili kujua
maumivu yake yanakuaje…baada ya kupata jibu akachukua maamuzi mazito.
Mwanaume huyo aliamua kujipiga risasi ya
mguu ili kuona inakuwaje na kujikuta mikononi mwa polisi na kukimbizwa
kwanza hospitali baada ya hali yake kuwa mbaya kabla ya kufunguliwa
mashtaka.
Pamoja na maumivu aliyokuwa nayo aliamua kuitupa bastola hiyo ili kufuta ushahidi kabla ya polisi kumfanyia uchunguzi wa kina.
Jamaa huyo alijitetea kwa polisi kuwa
aliamua kufanya kitendo hicho ili kujua mtu anayepigwa risasi huwa
anajisikiaje na bado upepelzi unaendelea ili kuweza kufunguliwa
mashtaka.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni