Ujumbe wa Ray C kwenda kwa watumiaji Madawa ya kuevya.
Good news kutoka kwake leo kupitia ukurasa wake wa Instagram ametoa taarifa kuhusu kufungua asasi ya kuwaelimisha vijana na jamii kuhusu madhara ya utumiaji wa madawan ya kulevya.
‘Ray C Foundation ni asasi ilioanza rasmi Feb 2014,nia na madhumuni ya hii asasi ni kuelimisha vijana na jamii yote kwa ujumla madhara ya utumiaji wa madawa ya kulevya kwani madawa ya kulevya ni tatizo kubwa sana lililoikumba nchi yetu ya Tanzania.
‘Palikuwepo na ukimya mkubwa juu ya haya madawa ya kulevya,majadiliano juu ya ulevi huu yalikuwa hayazungumziki kwa uwazi hata kidogo japo madhara ya matumizi ya dawa za kulevya ni makubwa sana na yanatisha katika jamii yetu hapa Tanzania…….Nia na madhumuni ya kuaznisha Ray C Foundation hasa ni kuhamasisha na kueleimisha vijana nan jamii nzima athari za utumiaji madawa ya kulevya na kuwafikia walengwa ndani ya jamii na katika maeneo yao nchi nzima!!!Eeh Mungu tuepushe na janga hili Nguvu kazi ya Taifa isipotee………
We need your Support…………
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni