Na hizi ndiyo sifa za simu mpya Samsung Galaxy S5
Biashara ya smartphone ni kubwa sana hivi sasa na karibia kila mwaka makampuni makubwa huwa yanakuja na simu mpya zenye ubora zaidi.
Samsung galaxy S5 ambayo inategemewa kuanza kuuzwa April 11 imetangazwa na kuonyeshwa kwa mara ya kwanza huko Barcelona kwenye Mobile world congress.
Baadhi ya sifa za simu hii mpya ni kuwa water and dust resistant, fingerprint,16 megapixel real camera and 2.1 megapixel front camera,4K video recording,screen ya Full High Definition Super AMOLED 1920 x 1080 (5.1 inches),RAM 2GB,Storage 16/32GB,Micro card SD up to 128GB,Operating System ni Android 4.4.2 Kitkat,Battery 2800mAh
Kitu kingine wanasema kwamba simu hiyo ina ultra power saving mode ambayo kwa mfano chaji ya simu yako imeisha na kubaki 10%, simu inazifunga kazi nyingine zote za simu na kubakisha sms na pia display inakuwa black and white nakuifanya hiyo 10% iliyobaki ukatumia simu kwa masaa 24 tangu hapo.
Kids mode: Kuna wakati watoto wanalilia simu yako kama ukiwa na S5 basi unaweka kids mode itafunga vitu vyote vya muhimu kwenye simu yako na kubadilisha muonekano(theme) hadi kuwa wakitoto ikijumisha games na vitu vingine kwa ajili ya watoto.
Kuwepo kwa finger print kwenye Samsung S5 inaweza kuendeleza msemo wa kusema wana-copy features za iPhone lakini matumizi ya fingerprint ni makubwa zaidi kwenye S5 zaidi ya iPhone.
Unaweza ku-swipe fingerprint yako mara moja na kuruhusu malipo kufanyika online hapohapo ukiwa unatumia S5. Hiyo fingerprint yako inahifadhiwa humohumo kwenye simu yako na sio kwenye cloud storage kwa hiyo hakuna ishu ya kuchukuliwa fingerprint yako.
Pia wanasema S5 imeongezwa uwezo kwenye ishu ya data switch (LTE Cat 4 na Wifi Mimo) zitakuwezesha ku-enjoy connection ya ajabu kwenye wireless na ukitumia kadi.Pia kuna kitu kipya kinaitwa download booster ambapo unaweza kutumia ku-download vitu kwa speed isiyo ya kawaida.
Ukichaji simu vizuri ikajaa kama inavyotakiwa unaweza kuitumia ku-surf kwenye internet kwa masaa 10 au kuangalia video kwenye simu yako kwa masaa 12.
Wale picha sasa hii simu ina chipset ambayo inasaidia camera kupiga picha za haraka sana kiasi kwamba unaweza kuzipata picha vizuri hata kama tukio linafanyika kwa haraka. Hii inakuwa fastest ever autofocus kwenye smartphone.
Unaweza pia kupiga picha kama zinazopigwa kwenye professional cameras ambapo unaweza kufanya refocus selection na kupiga picha yenye blur sehemu ya nyuma na kuonyesha clear sehemu ambayo umekusudia.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni