Unaambiwa huyu ni mwanasiasa mwenye umri mdogo kuliko wote duniani
Robert ‘Bobby’ Tufts hajaanza hata shule ya Nursery ambayo huku Tanzania tunaifahamu kama chekechea au vidudu lakini tayari ameshajiwekea historia ya kuwa mwanasiasa mwenye umri mdogo kuliko wote duniani .
Dogo huyo ameweza kuwa meya wa mji mmoja huko Minesotta akiwa na umri wa miaka mitatu pekee, unaambiwa ni Meya wa mji mdogo wa Dorset ulioko huko Minesotta Marekani na hii ni mara yake ya pili kuchaguliwa kuwa meya wa mji huo baada ya kupigiwa kura siku ya jumapili ambapo aliweza kushinda kipindi chake cha pili cha uongozi .
Mji huo una serikali ndogo inayoongozwa na meya huyo mdogo ambaye anaongoza idadi ya watu 220 ambao ni wakazi wa mji huo ambapo kama ilivyo kwenye manispaa yoyote, meya Bobby anaongoza serikali ambapo hufanya maamuzi yanayohusu bajeti ya matumizi ya mji wa Dorsett pamoja na masuala mengine nyeti kama ya kodi na makusanyo mengine ya mapato.
Mama mzazi wa Meya Robert Tufts, Emma Tufts anasema kuwa moja ya agenda za uongozi wa mwanaye ni kukusanya fedha kwa ajili ya taasisi ya misaada ya Ronald McDonald iliyoko Dorset eneo la Red River Valley Fargo Dakota ya Kaskazini pamoja na ujenzi wa kibao kipya cha kuwakaribisha wageni huko Dorset kwenye barabara zinazopakana na miji mingine.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni