T.I ashiriki kwenye ngoma iliyotengenezwa na msanii toka Kenya , video yake hii hapa.
Mwanamuziki na mtayarishaji wa muziki toka Kenya Lovy Longomba ambaye kwa muda mrefu sasa amehamishia makazi yake nchini Marekani ameanza kuonja matunda ya mafanikio kwenye industry ya muziki hasa ule wa kimataifa .
Hii ni baada ya kazi aliyoiandaa kutumika na mwanamuziki wa kimataifa toka nchini humo Clifford Harris Jr maarufu kama T.I ambaye ni rapa maarufu anayetokea huko Atlanta .
T.I amerap kwenye track ya rapa wa kike toka Australia Iggy Azalea akiwa ameshirikishwa na mwanadada huyo katika nyimbo ya Change Your Life ambayo imetengenezwa na Lovy Longomba .
Lovy Longomba ni mmoja wa wanandugu watatu waliokuwa wanaunda kundi la The Longombas ambalo liliwahi kutamba na ngoma kali kama vile Dondosa ambayo iliwahi kufanya vizuri kipindi cha mwanzoni mwa miaka ya 2000 wakiwa wanamuziki hao wakisimamamiwa na studio za Ogopa Djs .
Longomba kwa sasa amekuwa producer nchini Marekani na nyimbo ya Change Your Life ambayo ina siku tatu tangu ilipozinduliwa rasmi ambapo iliweza kutazamwa na watu 160,000 ndani ya saa 24 za kuzinduliwa kwake .
Lovy Longomba na ndugu zake wawili akiwemo Richie Richie Longomba ambaye alihamia nchini Tanzania kipindi Fulani ambapo alitoa nyimbo iliyvuma sana ya funguo wanatoka kwenye familia ya muziki ambapo marehemu baba yao Lovy Longomba alikuwa mwanamuziki maarufu nchini Kongo na baba yao mdogo Awilo Longomba anabaki kuwa moja ya Malegends wa muziki wa Afrika akiwa amewahi kutwaa tuzo ya Kora mwaka 1997 kama mwanamuziki bora wa kiume kwa mwaka huo . Pia Lovy Longomba alikuwa na mtoto wa kike aliyewahi kufanya muziki nchini Tanzania kama mnenguaji na baadaye mwimbaji kabla ya kufariki dunia aliyekuwa anaitwa Elly Longomba .
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni