YoungConciousâ„¢

Be Updated on the World of Sports, latest News and Entertainment Stories.

Propellerads

Breaking News

Translate

Welcome to Young concious .blogspot.com ==>>Feel free to leave your comment

Jumapili, 15 Septemba 2013

Bale aanza maisha mapya Real Madrid kwa Goli.


Winga mpya wa Real Madrid Gareth Bale alianza maisha yake ndani ya klabu hiyo kwa goli katika mchezo wake wa kwanza tangu aliponunuliwa kwa ada ya uhamisho iliyovunja rekodi .
Gareth alifunga moja kati ya mabao mawili ya Madrid wakati timu hiyo ilipotoka sare ya mabao mawili kwa mawili na Villareal .
Bao lingine la Madrid lilifungwa na Cristiano Ronaldo huku Villareal wakifunga kupitia kwa Giovani Dos Santos na Cani .
bale bale bale bale bale
bale bale bale bale
Wapinzani wa Real kwenye mbio za ubingwa wa Hispania Fc Barcelona ambao pia ni mabingwa watetezi walipata ushindi wa tabu katika mchezo wao dhidi ya Fc Sevilla .
Barca walishinda kwa mabao matatu kwa mawili wafungaji wakiwa Dani Alves , Lionel Messi na Alexis Sanchez huku Coke na Ivan Rakitic wakiwafunga mabao ya Sevilla .
Katika mchezo mwingine Atletico Madrid walipata ushindi wao wan ne kwa msimu huu baada ya kuwafunga Almeria kwa mabao manne kwa mawili .
 Ushindi huo unawafanya Atletico Madrid kuwa kileleni mwa ligi ya Hispania kama Barcelona wakiwa na rekodi za kufanana kwenye pointi , mabao ya kufunga na kufungwa.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

Propellerads