YoungConciousâ„¢

Be Updated on the World of Sports, latest News and Entertainment Stories.

Propellerads

Breaking News

Translate

Welcome to Young concious .blogspot.com ==>>Feel free to leave your comment

Jumatano, 12 Juni 2013

WAENDA KUFUNGA NDOA KWA BODABODA , WARUDI KWA MIGUU

Padri Phidelisi Mwesongo akiwafungisha
ndoa Charles Kanyema na Onoratha
Pascal .
Ibada ya wanandoa hao ikiendelea
kabla ya kurudi nyumbani kwa mguu .
Na Dustan Shekidele , Morogoro
WANANDOA Charles Kanyema (29 ) na Bi .
Onoratha Pascal ( 28) hivi karubuni
waliwashangaza wakazi wa Manispaa ya
Morogoro baada ya kwenda kufunga ndoa
wakiwa wamepanda bodaboda na kurejea
nyumbani kwa kutembea kwa miguu.
Ndoa hiyo iliyofungwa katika Kanisa
Katoliki Jimbo la Morogoro Mjini na
kufungishwa na Paroko Msaidizi , Padri
Phidelisi Mwesongo iligharimu shilingi
45,000 tu.
“Gharama hizo ni pamoja na picha 5 kwa
ajili ya kumbukumbu yetu na nyumbani
tumenunua mchele na nyama kwa ajili ya
sherehe ndogo ,” alisema bwana harusi
Kanyema.
Alisema fedha hizo zilitokana na michango
waliyochangiwa na wana jumuiya wenzao
na hawakutaka mambo makubwa katika
sherehe yao.
Mara baada ya kuwafungisha ndoa , Padri
Mwesongo aliwataka wanandoa hao
kutambua kwamba maisha ya ndoa ni
magumu na yanahitaji uvumilivu ili ndoa
yao iweze kudumu .
Baadhi ya watu waliohudhuria sherehe
hiyo waliwasifu wanandoa hao kwa
kutotumia gharama kubwa wakidai
kwamba mara nyingi ndoa zilizojaa kila
aina ya mbwembwe huwa hazidumu.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

Propellerads