YoungConciousâ„¢

Be Updated on the World of Sports, latest News and Entertainment Stories.

Propellerads

Breaking News

Translate

Welcome to Young concious .blogspot.com ==>>Feel free to leave your comment

Jumapili, 23 Juni 2013

MCHEZAJI WA CROATIA ALEN PAMIC AFIA UWANJANI Saturday

Wachezaji wa timu ya Crotia,
wakimsaidia mchezaji mwenzao, Alen
Pamic (aliyelala), wakimpatia huduma ya
kwanza na katika moja ya mechi
alizowahi kuzimia uwanjani hivi karibuni
kutokana na matatizo ya ugonjwa wa
moyo.
*************************************
***
Hivi karibuni, Pamic alipoteza fahamu
katika mechi ya ligi dhidi ya Lokomotiva
iliyopigwa Februari, ambapo licha ya
matatizo yake hayo alisisitiza kuendelea
kucheza soka, huku madaktari wake
wakimruhusu kufanya hivyo
NYOTA wa soka la kulipwa raia wa
Croatia, Alen Pamic ameanguka uwanjani
na kufariki dunia wakati wa mechi ndogo
isiyo ya kimashindano, gazeti la kila siku
la Vecernji List limesema katika toleo
lake mtandaoni la leo Jumamosi.
Taarifa hiyo imeripotiwa kwa ufupi,
huku ikiwa haina maelezo zaidi
kuhusiana na kifo cha Pamic aliyekufa
akiwa na umri wa miaka 23 tu.
Pamic, aliyekuwa akichezea klabu ya NK
Istra 1961 katika ligi ya daraja la juu
zaidi nchini hapa, alikuwa na historia ya
matatizo ya moyo, ambayo
yalimwangusha dimbani mara tatu kabla
ya tukio hilo lililochukua uhai wake.
Hivi karibuni, Pamic alipoteza fahamu
katika mechi ya ligi dhidi ya Lokomotiva
iliyopigwa Februari, ambapo licha ya
matatizo yake hayo alisisitiza kuendelea
kucheza soka, huku madaktari wake
wakimruhusu kufanya hivyo.
Pamic aliyekuwa kiungo mahiri dimbani,
aliutumia msimu mmoja wa 2010/11
kuchezea klabu ya Standard Liege ya Ligi
Kuu ya Ubelgiji, lakini klabu hiyo
ikamtema muda mfupi baada ya kupata
shambulio la moyo na kuzimia akiwa
mazoezini, gazeti la Vecernji limesema
katika taarifa yake.
Pamic ni mtoto wa nyota wa zamani wa
kimataifa wa Croatia, Igor Pamic,
ambaye kwa sasa anainoa klabu ya NK
Istra 1961 aliyokuwa akiichezea
marehemu.

SOURCE: Bongoclantz

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

Propellerads