YoungConciousâ„¢

Be Updated on the World of Sports, latest News and Entertainment Stories.

Propellerads

Breaking News

Translate

Welcome to Young concious .blogspot.com ==>>Feel free to leave your comment

Jumapili, 23 Juni 2013

HALI YA MANDELA NI TETE...ASHINDWA KUFUMBUA MACHO KWA SIKU KADHAA==>>Soma Hapa

Mzee Nelson Mandela ameendelea kuwa
katika hali mbaya hospitalini jana baada
ya kubainika kwamba gari la wagonjwa
lililombeba Rais huyo wa zamani wa
Afrika Kusini kwenda hospitali
limeharibika.
Gari hilo la wagonjwa mahututi
liliharibika wiki mbili zilizopita wakati
Mandela alipokuwa akikimbizwa kwenye
hospitali moja mjini Pretoria, na
kumwacha 'njiapanda' kwa dakika 40.
Rais huyo wa zamani wa Afrika Kusini
alihamishiwa kwenye gari jingine la
wagonjwa la hospitali ya kijeshi kumalizia
safari iliyobaki ya dakika 50 kati ya
Johannesburg na Hospitali ya Moyo ya
Medi-Clinic.
Msemaji wa Rais Mac Maharaj alisema:
"Tahadhari zote zimechukuliwa
kuhakikisha kwamba hali ya kiafya ya
rais wa zamani Mandela haiathiriki na
tukio hilo."
Madaktari wanaomtibu Mandela
waliridhika kwamba hakupata maumivu
yoyote katika kipindi hiki, aliongeza
Maharaj.
Taarifa ya jana kuhusu afya ya Mandela
inaonesha kwamba kuna mabadiliko
kidogo katika hali ya shujaa huyo wa
kupinga ubaguzi wa rangi tangu
alipopokelewa hospitalini hapo.
Mandela, ambaye alikuwa rais wa kwanza
mweusi wa Afrika Kusini mwaka 1994,
alikimbizwa hospitali moja ya Pretoria
mapema Juni 8 kufuatia maambukizi
kwenye mapafu.
Ilidaiwa jana kwamba Mandela
hajitingishi na familia yake sasa inajadili
uwezekano wa kusitisha matibabu.
Amekuwa hospitalini kwa wiki mbili
akipambana na maambukizi hayo, lakini
taarifa zilizopita zimeashiria kwamba afya
ya Mandela inaimarika.
Kwa mujibu wa vyanzo vipya, ufanyaji
kazi wa ini na figo za Mandela umeshuka
hadi asilimia 50 na hakufungua macho
yake kwa siku kadhaa.
Pia alitakiwa kufanyiwa oparesheni mbili
hivi karibuni, moja kutibu vidomda vya
tumbo zilivyokuwa vikichuruzika damu na
nyingine kuchomeka mpira mwilini
mwake, imeripotiwa.
Taarifa hizi zinaashiria kwamba suala la
Mandela ni kubwa kuliko inavyoripotiwa
na mamlaka za Afrika Kusini.
Historia ya matatizo ya mapafu ya
Mandela ilianzia tangu alipokuwa kwenye
gereza la Kisiwa cha Robben karibu na
Cape Town. Aliachiwa huru mwaka 1990
baada ya miaka 27 na akaendelea
kutumikia nchi kama Rais kuanzia mwaka
1994 hadi 1999.
Kulazwa kwake hospitalini ni mara ya nne
tangu Desemba, mwaka jana.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

Propellerads