YoungConciousâ„¢

Be Updated on the World of Sports, latest News and Entertainment Stories.

Propellerads

Breaking News

Translate

Welcome to Young concious .blogspot.com ==>>Feel free to leave your comment

Jumatatu, 24 Juni 2013

ANUSURIKA KIFO BAADA YA KUGONGA NYUMBA AKIJIFUNZA KUENDESHA GARI MORO

MWANAMKE mmoja ambaye jina lake
halikufahamika mara moja jana usiku
alinusurika kifo baada ya kugonga nyumba
wakati akijifunza kuendesha gari aina ya
Prado lenye namba za usajili T 952 BTJ .
Tukio hilo lilitokea majira ya saa tatu usiku
maeneo ya uwanja wa ndege jirani na Chuo
cha Ujenzi njia panda ya kuelekea gereji ya
Msuya.
Mbali na mwanamke huyo kunusurika kifo,
pia familia iliyokuwa ikiishi kwenye
nyumba iliyogongwa nayo ilinusurika
baada ya gari hilo kuvunja ukuta wa
nyumba na kuingia mpaka chumbani
ambako familia ilikuwa inajianda kulala.
Mashuhuda wa tukio hilo walipohojiwa na
mtandao huu walidai kwamba mwanamke
huyo ambaye bado hajaiva kwenye udereva
alikata kona iliyo eneo hilo kwa mwendo
kasi.
"Huyu mama anajifunza kama unavyoona
kibao cha ' L' kwenye gari yake , uzembe
alioufanya alikata kona hii kwa mwendo
wa kasi na kwamba badala ya kukanyaga
breki alikanyaga moto na kuzidisha kasi
ndipo alipogonga nyumba hii. " Alisema
shuhuda mmoja aliyejitambulisha kwa jina
la Jumanne Athuman.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

Propellerads