Rais wa Marekani Bw. Baraka Obama na
Mkewe wanatarajia kufanya ziara ya nchi
tatu barani Afrika itakayojumuisha nchi
za Senegal, Afrika ya Kusini na Tanzania,
Kuanzia tarehe 26 Juni hadi tarehe 3
Julai.
Katika ziara yake hiyo, Rais atawekea
mkazo umuhimu ambao Marekani
inauweka katika ushirikiano wetu wa kina
na unaoendelea kuimarika na nchi za
Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara
kupitia mipango mbalimbali ikiwemo ile
ya kuimarisha ukuaji wa uchumi,
uwekezaji na biashara, uimarishaji wa
taasisi za kidemokrasia na uwekezaji
katika kizazi kipya cha viongozi wa
Kiafrika.
Rais atakutana na viongozi mbalimbali wa
kiserikali, sekta binafsi na jumuiya huru
ya kiraia ikiwemo vijana ili kujadili ubia
wetu wa kimkakati katika ushirikano wetu
rasmi na masuala mengine ya kimataifa.
Ziara hii itadhihirisha dhamira ya dhati
ya Rais ya kupanua na kuimarisha
ushirikiano kati ya Marekani na watu wa
nchi za Afrika Kusini mwa Jangwa la
Sahara katika kuimarisha amani na
ustawi katika kanda hii na duniani kote
kwa ujumla
Translate
Jumatano, 22 Mei 2013
UJIO WA RAIS OBAMA NCHINI TANZANIA
About Young Concious
Soratemplates is a blogger resources site is a provider of high quality blogger template with premium looking layout and robust design. The main mission of templatesyard is to provide the best quality blogger templates.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni