YoungConciousâ„¢

Be Updated on the World of Sports, latest News and Entertainment Stories.

Propellerads

Breaking News

Translate

Welcome to Young concious .blogspot.com ==>>Feel free to leave your comment

Jumatano, 22 Mei 2013

MWAMUZI WA AFRIKA KUSINI KUICHEZESHA STARS MOROCCO

Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu
(FIFA) limemteua mwamuzi kutoka Afrika
Kusini kuchezesha mechi ya mchujo ya Kombe
la Dunia, Kanda ya Afrika kati ya Tanzania
(Taifa Stars) na wenyeji Morocco (Lions of the
Atlas).
Mechi hiyo ya kundi C itachezwa Juni 8
mwaka huu jijini Marrakech, Morocco kwenye
Uwanja wa Grand kuanzia saa 3 kamili usiku
kwa saa za Morocco. Mwamuzi
atakayechezesha mechi hiyo ni Fraser Daniel
Bennett.
Bennett atasaidiwa na Thusi Zakhele Siwela
pia wa Afrika Kusini, wakati mwamuzi msaidizi
namba mbili atakuwa ni Marwa Range kutoka
Kenya. Mwamuzi wa akiba (fourth official) ni
Lwandile Mfiki wa Afrika Kusini.
Kamishna wa mechi hiyo ni Robert Mangollo-
M’voulou wa Gabon wakati mtathimini wa
waamuzi (referee assessor) ni Charles
Masembe kutoka Uganda.
Taifa Stars ambayo iko chini ya Kocha Kim
Poulsen, na ikidhaminiwa na Kilimanjaro
Premium Lager tayari iko kambini katika
hoteli ya Tansoma ikiendelea kujinoa kwa ajili
ya mechi hiyo ambapo kabla itajipima na
Sudan (Nile Crocodiles) Juni 2 mwaka huu
jijini Addis Ababa, Ethiopia.
Ratiba ya mazoezi kwa timu hiyo ni kama
ifuatavyo;
Mei 22 Saa 10 jioni
Uwanja wa Karume
Mei 23 Saa 1 asubuhi na Saa 10
jioni Uwanja wa Karume
Mei 23 Saa 10
jioni Uwanja wa Karume
Mei 25 Saa 1 asubuhi na Saa 10
jioni Uwanja wa Karume
Mei 26 Saa 3
asubuhi                            Uwanja wa Karume

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

Propellerads