YoungConciousâ„¢

Be Updated on the World of Sports, latest News and Entertainment Stories.

Propellerads

Breaking News

Translate

Welcome to Young concious .blogspot.com ==>>Feel free to leave your comment

Jumatano, 29 Mei 2013

Mwanamke akatwa makalio, mikono na miguu yote kunusuru maisha yake baada ya kuchoma sindano ya kuongeza makalio.

Tamaa ya kutaka kurekebisha viungo na
muonekano aliokupa Mwenyezi Mungu eti ili
ufanane na flani inaweza kugeuka kuwa zaidi
ya hatari kama iliyomkuta mama huyu
aliyefahamika kwa jina la Apryl Michelle
Brown mwenye umri wa miaka 46 ambaye
ndoto yake ilikuwa kuwa na muonekano kama
wa Jennifer Lopez ama Janeth Jackson na
badala yake akajikuta kapoteza mikono, miguu
na sehemu ya makalio yake.
Mama huyo mkazi wa Los Angeles Marekani
alikua ni mfanya kazi wa saloon ya kike kwa
muda mrefu lakini maelezo ya mtaani na
kutamani kubadili umbo lake vilimponza na
baada ya kukaa kimya kwa muda mrefu tangu
alipoteza viungo vyake vya mwili aliamua
kujitokeza hadharani kueleza ili kuwanusuru
watu wengine.
Apryl ambae pia ni mama wa watoto wawili
alisema, “nahitaji kushare story yangu kwa
watu wengine ili kutoa onyo hasa kwa upasuaji
na matibabu ya haraka na haramu, mimi
sikujua hatari yake, nilidhani ni sindano isiyo
na madhara ambayo ingenipa makalio
niliyoyahitaji, kumbe haikuwa salama kwa
matumizi ya binadamu, baada ya kutumia
mwili wangu ulipata madhara makubwa
almanusura nipoteze maisha, niliteseka
nikafikia point nikaona kifo kingenipumzisha,
lakini njia pekee ambayo Daktari angeweza
kuyanusuru maisha yangu ilikuwa ni
kuniondoa sehemu ya makalio, kunikata miguu
yote na mikono.”
Mama huyo aliyesimulia mkasa wake kwa
masikitiko makubwa alijilaumu na kujutia kwa
kuwa alitumia pesa nyingi kukamilisha zoezi la
kuchoma sindano kwa watu wa mtaani
wanaofahamika kwa jina la “Pampers” ambao
hujiita madaktari wakiwa mtaani na kutoa
huduma kwa bei nafuu.
Alisema aliona rafiki zake wakiwa wamefanya
zoezi hilo na akaamini wamefanikiwa ndipo na
yeye akaamua kuchukua uamuzi ambao
mwisho wa siku uliyabadilisha kabisa maisha
yake.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

Propellerads