YoungConcious™

Be Updated on the World of Sports, latest News and Entertainment Stories.

Propellerads

Breaking News

Translate

Welcome to Young concious .blogspot.com ==>>Feel free to leave your comment

Jumatano, 29 Mei 2013

ZIJUE 'IDEAS’ 7 ZA JINSI YA KUANZISHA BLOGU ZENYE MVUTO, SOMA MAKALA HII KUTOKA MBUKE TIMES BLOG

Ukifuatilia sana fani ya blogging nchini kwetu
Tanzania, utagundua changamoto kubwa
iliyopo ni katika ubunifu na uandishi wa
taarifa za kuweka katika blogu. Tatizo la
ubunifu linajionyesha wazi kwa utitiri wa
blogu zenye mwelekeo mmoja kwamba nyingi
ni blogu za habari za matukio ya kila siku, na
kwamba habari zenyewe nyingi ni ‘copy &
paste’.
Imefikia hatua sasa, watu wengi kuchukulia
kuwa blogging ni jambo la kama vile mzaha
mzaha tuu,na kwamba mtu yoyote yule ili
mradi anajua kutumia computer ,ataweza
kufungua blogu yake na kuwa ana copy na ku
paste habari toka vyanzo mbalimbali na
kuweka kwa blogu yake.
Hata hivyo, bado kuna uwezekano mkubwa wa
watu wanaotaka kuanzisha blogs wakatumia
ubunifu kidogo kuboresha blogs zao kwa
kuleta upekee wa taarifa wanazoweka, na la
msingi sana tutazame thamani ya taarifa
tunazoweka kwa wasomaji wetu.
Tanzania ni yetu sote, na kwamba blogs zina
mchango mkubwa kama chombo cha habari
kuelimisha na kuelekeza jamii kwenye
muelekeo sahihi. Ni kweli kuwa picha za
utupu, na habari za udaku ‘zinauza sana’ lakini
tukumbuke kuna mambo mengine mengi tuu
ambayo tungeweza kuandika kama bloggers na
kutoa mchango kwa jamii yetu.
Kuna msemo unaosema “ Be change you want
to see” Yaani wewe mwenyewe uanze kwanza
kufanya mabadiliko kabla ya kudai mabadiliko
yatokee tuu.
Zifuatazo ni baadhi ya ‘ideas’ ambazo zinaweza
kutengeneza blogs zenye ‘kuuza’ (kuleta
wasomaji wengi) na pia zikaleta mchango
chanya katika jamii. UPO HURU KUTUMIA

‘IDEAS’ HIZI KUTENGENEZA BLOGU YAKO

1.Fursa kwa wajasiriamali : Waweza anzisha
blogu mahsusi kwa fursa motomoto kwa
wajasiriamali wa sasa na wale wanaotaka kuwa
wajasiriamali. Blogu hii haitojihusisha na
makala kuhusu ujasiriamali (maana wapo
wengi wanaandika kuhusu hilo) badala yake
itajikita katika kuweka taarifa motomoto za
upatikanaji wa mafunzo ya ujasiriamali,
mikutano, semina, mikopo, na asasi
mbalimbali zinazosaidia wajasiriamali. Waweza
pia weka links za blogs zinazohusiana na
ujasiriamali ili kufanya blogu hii iwe nyumbani
kwa wajasiriamali.

2. Shule za Kata: Habari nyingi zinaandikwa
kuhusu shule za kata. Ili kuleta upekee blogu
yako hii itajikita kueleza mafanikio ,
changamoto na jinsi shule za kata
zinavyojitahidi kujikwamua. Takwimu na picha
ni muhimu sana kwa blogu hii. Pia unaweza
onyesha program mbalimbali za maendeleo
zinazosaidia shule za kata. Kuhoji wanafunzi
wa shule husika, na kuonyesha maisha ya
shule za kata. Lengo ni kusaidia wazazi na
walezi kutambua mazingira na maendeleo ya
shule wanazopeleka watoto wao, au
wanazotarajia kupeleka watoto wao. Maana
wapo wengi mtoto toka Form 1 hadi Form 4,
hawajakanyaga shule anaposoma mtoto.

3.Picha Uwanjani: Kuna blogu nyingi zenye
habari na michezo na burudani. Ili kuleta
upekee, blogu yako hii itakuwa ni ya picha
tuu. Tena picha kali zaidi , ikisindikizwa na
Facebook page, yenye kusheheni picha za
matukio mbalimbali ya burudani na michezo.
Si unajua kuwa picha inatoa maneno maelezo
zaidi ya Maneno ? Ndio hivyo, hakikisha picha
unazoweka zinabeba ujumbe au taarifa fulani,
ambayo hautoelezea kwa maneno ila
mtazamaji atajionea mwenyewe. Kumbuka
kutaja vyanzo vya picha ambazo haukupiga
wewe mwenyewe.

4.Nukuu zetu: Unakumbuka nukuu kama vile
“…ukitaka kula ukubali kuliwa”?. Basi waweza
tengeneza blogu maalum ya nukuu toka
Tanzania. Waweza zigawa katika makundi ya
Siasa, Jamii, Teknolojia, Uchumi, Michezo,
Elimu, n.k. Usisahau ile nukuu ya Tanzania ni
muungano wa visiwa vya Zimbabwe, Pemba na
Tanganyika. Kumbuka kupata nukuu sahihi, na
ikiwezekana utaje kabisa nani alitoa maneno
hayo. Blogu hiyo ya nukuu zetu, itaburudisha
na kuelimisha pia, na kutukumbusha wapi
tunatoka, na wapi wapi tutarajie kuenda.

5.Skonga: Blogu hii itakuwa maalum kwa
wanafunzi na wazazi. Ni kama vile shule, ila
shule ya mtandaoni, ambapo Matokeo
mbalimbali ya Form 4, 2, QT, FORM4,
yatawekwa. Msaada kwa wanafunzi kwa njia ya
‘materials’ ya kujisomea yataweka, na makala
zenye kujaa mbinu za kusoma, changamoto za
maisha ya kishule, habari motomoto zihusuzo
elimu zitawekwa humu. Mambo mengine ya
maisha ya kishule kama vile majina ya walimu,
ambayo wanafunzi huwatunga yatawekwa
humu.

6.Wakali wa Bongo: Badala ya kuandika
habari za watu maarufu na mashuhuri kama
udaku, blogu hii ya wakali wa Bongo,
itajitofautisha kwa kuangalia maisha ya watu
hawa katika muonekano chanya. Blogu
itachambua changamoto wanazokumbana
nazo, nini wamejifunza kuhusu mafanikio, na
wanafanya nini kuendelea kubaki kuwa na
mafanikio. Pia blogu itaangalia wakali wengine
waliopo katika jamii lakini hawajapata kuwa
mashuhuri kama vile wanafunzi waliofaulu kwa
viwango vya juu kabisa katika masomo yao.
Itaangalia pia biashara zinazotamba Tanzania,
Shule zinazotamba na zilizowahi kutamba
kama vile TAMBAZA, wanasiasa, na asasi zisizo
za kiraia. Blogu hii itanogeshwa na mahojiano
na wahusika, picha, na historia mbalimbali.
Unataka kuanza blogu hii ? Embu fuatilia na
kuandika ukali wa shule ya TAMBAZA. Enzi
hizo TAMBAZA ilivyosifika kwa fujo lakini pia
kwa ubora wa wanafunzi.

7.Mkali wa Facebook: Blogu hii ni mahsusi
kwa mambo yanayovutia kuhusiana na
Facebook. Mambo kama vile picha zilizopata
‘likes’ nyingi (zisiwe picha za mtu binafsi),
status kali, au comments zenye mvuto zaweza
kuwekwa humo. Mambo mengine ni taarifa za
kiufundi kuhusu applications mbalimbali
zinazopatikana Facebook kama vile BranchOut,
na mambo mapya ya matumizi ya Facebook
yanayoletwa na kampuni ya Facebook kama
vile Timeline.

CHANZO : BONGOCLANTZ.COM

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

Propellerads