Siku chache baada ya kuondoa stress za
mahusiano ya mapenzi juu ya Selena Gomez
‘The Beauty and beat singer’ Justin Bieber
amekumbana na matatizo mengine ambayo
yanaweza kuwa makubwa zaidi ya stress
alizokuwa nazo, baada ya kuwa kero kwa
majirani zake ambao wanajuta kukaa karibu na
staa huyo kwa kuwa tabia zake zimeuharibu
utulivu uliokuwepo katika ujirani huo huko
Los Angeles.
Majirani hao wameiambia TMZ kuwa Bieber na
marafiki zake wamekuwa wakisababisha kelele
nyingi usiku wa manane wanaporudi kutoka
viwanja na kuendesha gari lake aina ya Ferrari
kwa fujo na wakati mwingine pikipiki yake,
lakini pia hata wakifikika nyumbani
huendeleza party huku wakiachia sauti juu na
kuwanyima usingizi majirani hao.
Majirani hao walisema mida ya mchana Bieber
hupita na gari lake taratibu mbele ya watoto
wadogo huku akivuta marijuana a.k.a bangi
waziwazi, na kwamba siku moja mwimbaji
huyo alikuwa anaendesha akiwa na rafiki yake
ambae pia alikuwa anavuta bangi.
Walisema hata bodi ya mmiliki wa nyumba
hizo imewaambia majirani hao kuwa
amepanga kuripoti polisi suala hilo kwa kuwa
ni swala la kiharifu na linalovunja haki za
msingi za majirani hao. Majirani hao pia
wamesharipoti polisi tayari na polisi
wamepanga kuzuia uendeshaji magari mida ya
usiku sana katika maeneo hayo ili kuondoa
kero hizo.
Mkasa huu uliompata wa kuchukiwa na
majirani zake unaweza kufanana kidogo na ule
wa Chris Brown kushtakiwa na majirani zake
kwa kuwa alichora michoro iliyosemekana
kuwatishia watoto wao. Lakini hii ya Bieber
kuvuta marijuana mbele ya watoto wao
itakuwa imetisha zaidi.
Translate
Jumatano, 29 Mei 2013
Home
/
Unlabelled
/
Justin Bieber awa kero kwa jirani
zake, wamtuhumu kuvuta bangi
mbele ya watoto na kupiga kelele
usiku wa manane
Justin Bieber awa kero kwa jirani zake, wamtuhumu kuvuta bangi mbele ya watoto na kupiga kelele usiku wa manane
About Young Concious
Soratemplates is a blogger resources site is a provider of high quality blogger template with premium looking layout and robust design. The main mission of templatesyard is to provide the best quality blogger templates.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni