Kampuni ya kuunda magari ya Japan, Toyota imetangaza kuwa inaunga mkono kundi la waandisi ambalo linaunda gari linaloruka.
Toyota itataoia kima cha dola 300,000 kwa kundi hilo ambalo huendesha shughuli zake nje ya mji wa Toyota kati kati mwa Japan.Kundi hilo limekuwa likipata michango kugharamia kuundwa kwa gari hilo linalotumia teknolojia ya ndege zisizokuwa na rubani na linatajwa kuwa gari dogo zaidi linaloruka kuwai kuundwa.
Kundi hilo linaamini kuwa magari hayo yatatumiwa kuwasha mwenge wa olimpiki wakati mji wa Tokyo utaandaa mashindano ya majira ya joto mwaka 2020.
Source:BBCSwahili
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni