Meneja wa zamani wa Villarreal na Sevilla Marcelino Garcia Toral ameteuliwa kuwa meneja mpya wa klabu ya Valencia ya Uhispania.
Marcelino atakuwa meneja wa sita kuajiriwa na mmiliki wa klabu hiyo Peter Lim katika kipindi cha miaka miwili.
Marcelino ametia saini mkataba wa miaka miwili katika klabu hiyo ambayo imewahi kufika fainali Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya mara mbili.
Kaimu meneja Voro ataongoza klabu hiyo kwa mechi mbili zake zilizosalia msimu huu, ugenini dhidi ya Espanyol Jumamosi na nyumbani dhidi ya Villarreal 21 Mei.
Valencia wanashikilia nafasi ya 13 La Liga, karibu na eneo la kushushwa daraja badala ya nafasi ya kufuzu kwa ligi kuu za klabu Ulaya.
Valencia walianza msimu na kocha msaidizi wa zamani wa Liverpool Pako Ayestaran lakini akafutwa klabu hiyo ikishikilia mkua la Liga baada ya kushindwa mechi nne za wkanza ligini.
Marcelino, 51, alipigiwa upatu kuchukua nafasi ya Ayestaran.
Hata hivyo, sheria za soka Uhispania haziruhusu meneja asimamie zaidi ya kalbu moja msimu mmoja na hivyo hangepewa kazi wakati huo.
Ilihesabiwa kwamba alianza msimu akiwa Villarreal, ingawa alifutwa Agosti kabla ya mechi ya kwanza ya msimu.
Meneja wa zamani wa timu ya taifa ya Italia Cesare Prandelli, 59, alichukua usukani lakini akajiuzulu baada ya kuwaongoza mechi kumi.
Voro alichukua usukani lakini amesema ataondoka mwisho wa msimu.
Beki wa zamani wa Manchester United na England Gary Neville, 42, alifutwa na Valencia baada ya kuwa kazini chini ya miezi minne Machi 2016
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni