YoungConciousâ„¢

Be Updated on the World of Sports, latest News and Entertainment Stories.

Propellerads

Breaking News

Translate

Welcome to Young concious .blogspot.com ==>>Feel free to leave your comment

Ijumaa, 12 Mei 2017

Betri inayojaa chaji kwa dakika tano yaanza kuuzwa

StoreDot
StoreDot walitoa mfano wa siku ikiwekwa chaji kwa kutumia chaja maalum
StoreDot Image caption
Betri za simu za kisasa za Smartphone ambazo zinaweza kujaa chaji katika muda wa dakika tano pekee huenda zikaanza kuuzwa sokoni mwaka ujao.
Teknolojia hiyo iliwekwa kwenye maonesho mara ya kwanza mwaka 2015 na kampuni ya Israel ya StoreDot.
Kampuni hiyo iliwasilisha kwenye maonesho ya kila mwaka ya teknolojia mpya ya CES mjini Las Vegas betri hiyo maalum iliyopewa jina FlashBattery.
Afisa mkuu mtendaji wa kampuni hiyo Doron Myersdorf ameambia BBC kwamba sasa wanatarajia kuanza kuzalisha na kuuza betri hizo mapema mwaka 2018.
Hata hivyo, Ben Wood, mchanganuzi wa teknolojia katika kampuni ya CCS Insight amesema ana shaka kidogo kuhusu ahadi hiyo.
Bw Myersdorf amesema hawezi kufichua kwa sasa ni kampuni gani ambazo zimepata idhini ya kutengeneza betri kwa kutumia teknolojia hiyo.
Mwaka 2015, aliambia BBC kwamba betri hizo za kampuni yake zimeundwa kwa kutumia viungo ambavyo vinawezesha kufanyika kwa shughuli za kemia kwa haraka isiyo ya kawaida na pia kuhamishwa kwa nguvu za umeme kutoka sehemu moja hadi nyinginwe kwa kasi sana.
Baadhi ya miundo ya betri hizo ilikuwa kubwa kuliko betri nyingi za smartphone za wakati huo, lakini Bw Myersdorf anadai sasa wameandaa betri ambazo zinaweza kuanza kuuzwa sokoni.
"Tutachaji simu ya smartphone kwa dakika tano," alisema.
Aliongeza kwamba teknolojia hiyo tayari inafanyiwa majaribio na watengenezaji betri wawili China na kwamba utengenezaji kwa wingi wa betri hizo unatarajiwa kuanza robo ya kwanza ya 2018.
Lakini ingawa Bw Wood ana shaka kwamba betri hizo zinaweza kuuzwa haraka hivyo, amekiri kwamba iwapo betri hizo zitafanya kazi kama ilivyoahidiwa, basi utakuwa ni ufanisi mkubwa sana katika sekta hiyo.
"Kubahatisha kuhusu teknolojia ya betri kunaweza kukudhuru. Nimejifunza kuwa na shaka kila wakati kuhusu ahadi hizi. Hebu tusubiri," aliambia BBC.
Alieleza kuwa muundo wowote ambao unatoa joto kwa wingi unaweza kuathiri utendakazi wa betri.
 
StoreDot battery car
StoreDot pia wanadai wameunda betri ya gari inayoweza kujaa chaji kwa dakika tano pekee
Kuna kampuni nyingine zinazojizatiti kuunda betri ambazo zinajaa chaji kwa haraka.
Novemba, Qualcomm walitangaza betri za Quick Charge 4 ambazo zinaahidi betri hiyo itajaa chaji kwa dakika tano na kusalia na chaji kwa saa tano.
StoreDot pia walizindua betri ya gari ambayo inajaa chaji kwa dakika tano katika maonesho ya teknolojia mjini Berlin wiki hii.

Source:BBCSwahili

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

Propellerads