Utawala wa Urusi umekanusha vikali madai kwamba wamekuwa wakiiingilia kampeini zinazoendelea za uchaguzi wa urais nchini Marekani.
Shirika la kijasusi la Marekani,FBI linachunguza madai kiwa Urusi ilihusika katika kisa ambapo barua pepe kutoka chama cha Democratic zilidukuliwa.
Barua pepe hizo zinadaiwa zilinuiwa kumdhalilisha aliyekuwa anawania uteuzi wa urais kupitia tikiti ya chama hicho Bernie Sanders hivyo kuleta mgawanyiko baina ya wafuasi wake na wale wa Bi Hillary Clinton.
Tuhuma ni kwamba Urusi kisiri inamuunga mkono mgombea wa chama cha Republican Donald Trump na tayari rais Rais Obama amelizungumzia akisema kuna uwezekano mkubwa hilo ni kweli madai ambayo Urusi imekuwa ikiyakana .
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni