Wewe ni mmoja wa mateka wa simu?
Mji wa Augsburg umeweka taa za barabarani chini |
Watu wengi duniani, hasa vijana, wamegeuzwa watumwa na simu za mkononi na huwa vigumu sana kwao kuweka simu zao chini.
Hili hufanyika hata wanapotembea barabarani na wataalamu wanaonya kwamba hilo limechangia ongezeko la ajali barabarani katika miji mingi.Si ajabu kwamba katika mji wa Augsburg, Ujerumani wasimamizi wa baraza la jiji wameanzisha mfumo mpya wa kuweka taa za barabarani. Badala ya kuwekwa kwenye milingoti, taa hizo zinawekwa chini ili watu waweze kujua taa zikibadilika bila kuinua vichwa vyao.
Tatizo hilo la watu kutumia sana simu kiasi cha kutotaka kujishughulisha na mambo mengine limepelekea kubuniwa kwa msamiati mpya ambapo waraibu wa hilo wanaitwa Masmombi.
Dhana hii ya zombi imeunganishwa na jina la simu za kisasa ambazo kwa Kiingereza hujulikana kama smartphone.
Tumewauliza baadhi yenu iwapo mmekabiliwa na tatizo hili la kutumia sana simu na wengi katika ukurasa wetu wa Facebook na katika Instagram wanakubali kwamba hili ni tatizo kubwa.
Keisi Ahuura kutoka Entebbe Uganda amesema: "Kwa kweli Mimi ni #smombi wa daraja la juu. Mda mwingi zaidhi nakuwa kwa net sio kupiga simu.”
Said Mahseen naye anasema hawezi kukaa bila simu mkononi.
King Majuto pia anakiri kutumia simu sana, ila anasema alijaribu kupunguza akashindwa.
Katika kujaribu kuacha uraibu huu, Zakayo Samsom kwenye Instagram anasema alijiwekea malengo ya kuacha kununua kifurushi cha data.
"Kidogo ilisaidia,” anasema.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni