Stori kwenye U Heard ya clouds FM March 1 2016 ilikuwa ni hii ya staa wa bongoflevaBaraka da Prince, kuhusiana na tuhuma za kumtelekeza mtoto, Soudy Brown alipiga stori na msichana ambaye anadaiwa kupata mtoto na Barakah na kuelezea kuwa>>
‘tatizo sasa hatoi huduma ya mtoto, yani kila siku nikimpigia simu yuko busy anadai yuko studio na huku nyumbani kwetu wananifukuza wanadai niende Dar es salaam‘
Baada ya hizi stori, AYO TV ilimtafuta Barakah da Prince ili kupata ukamilisho ‘Kwanza siwezi kumkataa wala kumtelekeza mtoto, ni kweli mimi nina mtoto na taarifa za kuwa sitoi matumizi ya mwanangu‘
‘sijawahi kupewa taarifa za matumizi ya mwanangu na nikaachi kutuma, imeniumiza sana, na hii imeniuma kuliko kitu chochote kilichowahi kuniuma katika maisha yangu ‘ Barakah da Prince
Unaweza kumtazama hapa Barakah da prince akielezea maumivu hayo….
Source:MillardAyo
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni