Baada ya katibu Mkuu wa CUF Maalim Seif Sharif kurejea
kutoka India alipokuwa anafanyiwa upasuaji wa Mgongo na kwa mujibu wa
Daktari wake upasuaji ulifanikiwa na aliporejea alikuwa na afya njema na
akapumzika Zanzibar.
Leo March 8 2016 Maalim Seif Sharif amethibitisha
jana hali yake ilibadilika ghafla akiwa uwanja wa ndege Zanzibar,
alipata kizunguzungu kikali ikabidi asaidiwe kupelekwa kupanda ndege
kutoka Zanzibar mpaka Dar es salaam na kisha kulazwa hospitali na
leo ameyazungumza haya…
>>>nilipofikishwa
hapa walikuwa washajitayarisha wamenipokea vizuri sana wakaanza kufanya
uchunguzi wao na baada ya muda kama saa mbili tatu hali ikarudi
ikatengamaa, nikalala salama usingizi mzuri na nimeamka salama asubuhi
nimefanya mazoezi kwa miguu yangu mwenyewe na ninatembeatembea kwa miguu
yangu mwenyewe, hali sasa hivi ni nzuri kama kama kawaida‘:-Maalim Seif Sharif
Daktari wa Maalim Seif Sharif, Omary Mohamed Suleiman amethibitisha pia kuwa afya ya kiongozi huyo kuwa ni njema na muda wowote madaktari watamruhusu..
>>’hakuna
kubwa lililoonekana kila kitu kipo sawa, isipokuwa inaonekana ni hali
ya uchovu alihitaji mapumziko zaidi na baada ya kufika hapa Hospitali
madaktari baada ya uchunguzi wao wakaona bora abakie hospitalini wazidi
kumuangalia mpaka kesho yaani leo mpaka sasa hivi hali imeenda vizuri
tunategemea wakati wowote ataruhusiwwa kwa mujibu wa madaktari‘:-Omary Mohamed Suleiman
Source:MillardAyo
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni